Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amewakashifu viongozi wa serikali - Citizen TV Kenya
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amewakashifu viongozi wa serikali wanaoendeleza kampeni ya kuwataka vijana wapigwe risasi akisema mauaji ya vijana zaidi ya 40 wakati wa maandamano ya saba saba na maandamano ya awali ni ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Aidha Kalonzo amesistiza kuwa upinzani hautokubali mazungumzo yeyote na serikali, akaitaka serikali kutimiza ahadi alizotoa kwa wananchi.