Watu 4 wafariki na wengine waugua Changamwe, Mombasa
Watu wanne wamefariki dunia huku wengine wakiwa wamelazwa hospitali mbalimbali mjini Mombasa kufuatia ugonjwa usioeleweka katika mtaa wa matangini migadini eneo hilo. Waliofariki wameripotiwa kufura na kuchibuka mwili kwa malengelenge yanayotumbua maji huku sasa serikali ya kaunti ya Mombasa ikisema inafanya uchunguzi.