Waathiriwa wawili wa maandamano ya hivi karibuni ya saba saba wamezikwa
Waathiriwa wawili wa maandamano ya hivi karibuni ya saba saba wamezikwa katika hafla za mazishi zilizosheheni wito wa haki. Bridgit Njoki, msichana wa miaka 12 aliyefariki baada ya risasi kupenya ukutani na kumfikia alipokuwa sebuleni nyumbani kwao, alizikwa eneo la Githinguri, kaunti ya Kiambu huku Joseph Kagiri, wa miaka 24, naye akizikwa eneo la Ndeiya, kaunti hiyo.