Viongozi wa upinzani wavamiwa eneo la Chwele katika ziara ya Maghaibi

5 hours ago 3


Msafara wa Viongozi wa Upinzani ulishambuliwa na wahuni ambao walirusha mawe na kuharibu magari ya wanasiasa hao katika eneo la chwele Kaunti ya Bungoma katika siku ya pili ya ziara yao magharibi mwa nchi. Vijana walionekana kutupa mawe na kuharibu magari ya viongozi wakiwemo Kalonzo musyoka, Eugene wamalwa, Fred Matiang'i na Gavana wa Transzoia George Natembeya. Viongozi hao wamemnyoshea kidole cha lawama Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula kwani tukio hilo lilifanyika katika ngome yake ya kisiasa wakati ambapo ubabe wa kisiasa kati yake na Gavana Natembeya ukishamiri kuhusu nani ana ushawishi mkubwa eneo la magharibi mwa nchi.
Open Full Post