Idara ya polisi inafanya tathmini kuhusu tukio la Alhamisi ambapo kituo cha polisi cha mawego huko homa bay kiliteketezwa. Afisa mmoja wa ngazi ya juu ya idara hiyo ameiambia runinga ya Citizen kuwa uamuzi wa kujenga upya kituo hicho utafanywa kwa mashauriano na wakazi wa eneo hilo. Kwa sasa, maafisa wa polisi waliokuwa wakihudumu mawego wamehamishiwa hadi Kendu Bay.
Uchunguzi wafanywa kuhusu kuchomwa kwa kituo cha polisi cha Mawego