Siasa mitandaoni
MITANDAO YA KIJAMII WIKI HII IMEFURIKA PICHA ZA AKILI UNDE NA VIDEO ZA KUPINGA, KWA UCHESHI AMA KUKEJELI AMRI YA RAIS WILLIAM RUTO YA KUWAPIGA RISASI MIGUUNI WAANDAMANAJI WANAOLETA FUJO KWENYE MAANDAMANO. HALI HII YA KUTUMIA MITANDAO KISIASA IMESHIKA KASI, HASWA BAADA YA WIMBI LA GEN Z LA KUPINGA MSWADA WA FEDHA WA MWAKA WA 2024, NA INAELEKEA MOTO HUO HAUZIMIKI HIVI KARIBUNI