Serikali ya kaunti ya Kilifi imeanzisha ujenzi wa barabara za mjini
Serikali ya kaunti ya Kilifi imeanzisha ujenzi kadhaa wa barabara ambazo ni muhimu katikati usafiri na shughuli za kila siku katika mji wa Malindi hasa sekta ya uchukuzi. Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo, Afisa mkuj katika idara ya barabara na miundomsingi kaunti hiyo Philip Charo amewataka wenyeji kutunza raslimali ya kaunti ili waweze kunufaika hata zaidi. Charo aidha amewataka wakaazi kujitokeza katika vikao vya kutoa maoni ili serikali iweze kutatua changamoto zao kupitia Kwa miradi ifaayo. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na mwakilishi wa wadi ya shela aliyeisifia miradi hiyo na kuitaja yenye suluhu Kwa wachukuzi eneo hilo.