Redio Citizen yatua Bungoma, wazazi waaswa huhusu maadili - Citizen TV Kenya
Watangazaji wa Redio national leo walishiriki ibada ya jumapili katika kanisa la Holygate of Heaven kaunti ya Bungoma. Hii ni katika msururu wa misafara ya watangazaji wa Redio Citizen kutangamana na wafuasi wao maeneo mbalimbali nchini Akiongoza msafara huu, Mkuu wa Redio Citizen Tinah Ogal ameahidi kuwa kituo hiki kitaendelea kukuza matangazo na burudani zake kwa mashabiki. Waliozungumza wote wakigusia haja ya wazazi kuimarisha malezi mema kwa wana wao. Aidha, msafara huu umejumuisha kampuni ya Unga ya Joy Millers ambayo iliendelea kupigia debe chapa zake.