Rais William Ruto ameyataka mataifa yaliyoimarika kiuchumi duniani kulitizama bara la Afrika kama uwanja mkubwa wanaoweza kuwekeza, ili kusaidia kuboresha maisha ya zaidi ya watu bilioni 1.5, kupitia mali yake ghafi ya madini. Rais aliyezungumza kwenye mdahalo wa Afrika jijini London, amesema njia hii itayasaidia mataifa kama vile Kenya kupunguza madeni inayohitaji kukopa ughaibuni kufanikisha maendeleo. Na kama njia ya kuwavutia wawekezaji, Rais vile vile ametangaza kupanuliwa kwa soko la hisa nchini, kufuatia hatua ya ubinafsishaji kati ya mashirika ya serikali ambayo yanahitaji uwekezaji mkubwa kuyafufua na kuyaimarisha
Rais Ruto ayataka mataifa yaliyostawi kuwekeza Afrika