Rais Ruto amewaonya viongozi wa kidini na wa kisiasa
Rais William Ruto amewaonya viongozi wa kidini na wa kisiasa akisema kuwa wanachochea maandamano ya vijana nchini. Rais amesema kuwa matukio yanayoendelea nchini yametokana na uchochezi wa viongozi hao kwa kisingizio kuwa wanatekeleza haki yao ya kikatiba. Pia rais amesisitiza kuwa serikali itawachukulia hatua kali wanaovuruga amani pamoja na wanaofadhili maandamano hayo, sawia na wanavyokabiliana na magaidi.