Polisi wanachunguza kuteketezwa kwa kituo Itibo kaunti ya Nyamira
Maafisa wa polisi mjini Nyamira wameanzisha uchunguzi baada ya wakaazi kuteketeza kituo cha polisi cha Itibo kwa ghadhabu ya kupigwa risasi na kuuawa kwa kijana wa miaka 19. Kijana huyo aliuawa wakati wa maandamano siku ya Jumanne wakati wanafunzi wa chuo cha kiufundi cha Nyamira kuandamana wakilalamikia barabara mbovu eneo hilo