Omtatah alaani ongezeko la chuki za kikabila
Seneta wa Buais Okiya Omtatah amelaani vikali ongezeko la chuki za kikabila zinazoendelezwa na baadhi ya viongozi nchini. Omtatah anaonya kuwa semi za viongozi zinahatarisha ushikamano wa kitaifa na zinaweza kulirudisha taifa kwenye makovu ya uchaguzi wa 2007. Omtatah amepuuzilia mbali madai kwamba maandamano yanayoongozwa na kizazi cha Gen Z yamechochewa na ukabila, akisisitiza kuwa harakati hizo zinatafuta uwajibikaji, haki, na utawala bora bila kuzingatia kabila.