Naivas imeadhimisha miaka 35 kwa mbwembwe - Citizen TV Kenya
Duka kuu ya Naivas limeadhimisha miaka 35 kwa hafla maalum ya kuwashukuru wateja aftermath katika matawi yake yote nchini. Mkurugenzi Mkuu wa duka hilo David Kimani ametaja uaminifu wa wateja na imani ya jamii kama sababu kuu zilizofanya maduka hayo kukua, akisisitiza dhamira ya kuendelea boresha huduma zake kwa wateja. Kwenye mbwembwe hizo, wateja walipata zawadi kemkem huku Naivas ikisema kuwa sherehe hizo ni sehemu ya juhudi za kutoa shukrani kwa jamii na kutambua mchango wa wateja wake. Naivas ilianzishwa mwaka wa 1990.