NACADA yapendekeza kuongezwa kwa umri wa matumizi ya vileo
Wakenya wenye umri chini ya miaka 21 huenda wakakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kunywa pombe mara tu mpango uliopo sera ya taifa ya mwaka 2025 kuhusu pombe, dawa za kulevya na vileo utatekelezwa. Sera hiyo iliyoidhinishwa na baraza la mawaziri pia inataka serikali ipige marufuku uuzaji wa pombe kupitia mitandao.