Mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi IEBC- Erastus Ethekon aahidi uchaguzi huru na haki
Mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi IEBC- Erastus Ethekon ameahidi kuheshimu uamuzi wa wakenya kwenye uchaguzi mkuu wa 2027 na chaguzi zingine zitakazoendeshwa na tume hiyo. Akizungumza baada ya kuapishwa kwa makamishna wapya wa tumehiyo, ethekon aliazimia kurejesha imani ya wakenya kwa tume hiyo kwa kuwajibika na kufanya kazi kwa uwazi.