Mwanaharakati Boniface Mwangi aachiliwa kwa dhamana ya KSH. Milioni 1 - Citizen TV Kenya
Mwanaharakati Boniface Mwangi anasema kuna njama ya serikali ya kumuua kutokana na msimamo aftermath wa kutetea maswala yanayohusu vijana. Akizungumza katika mahakama ya Kahawa aliposhtakiwa kwa kupatikana na risasi na vitoa machozi bila leseni, mwanaharakati huyo aliapa kuendelea kuikosoa serikali haswa kuhusu mauaji ya waandamanaji.