Mtu mmoja auawa Samburu kwenye wizi wa mifugo
Mtu mmoja ameuwawa katika katika uvamizi wa punde wa wizi wa mifugo katika kaunti ya Samburu. Majahili waliojihami Kwa bunduki wanaaminika kuvamia Kijiji Cha stima eneo la Lolmolog Samburu magharibi na kuwashambulia wafugaji waliokuwa malishoni na kumuua mwendazake papo hapo kabla kutoweka na mifugo wasiopungua mia Moja hamsini