Msongamano wa wanafunzi katika shule ya Mwaghogho

5 days ago 2


Kufuatia kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi katika shule ya upili ya Mwaghogho eneo bunge la Voi, hazina ya ustawishaji eneo bunge hilo imejenga bweni katika shule ya upili ya Mwaghogho kwa shilingi milioni 15. Mbunge wa Voi Khamisi Chome akisema kwa muda wanafunzi wamekosa malazi bora katika shule hiyo licha ya kuongoza kwa miaka miwili mtawalia katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne. Aidha wazazi na waalimu eneo hilo wakisema watashirikiana ili kuimarisha elimu hasa wakati ambapo mgao wa fedha kwa wanafunzi unatolewa na serikali mara nyingi huchelewa.
Open Full Post