Msafara wa MPESA sokoni leo umekuwa Rift Valley
Msafara wa Mpesa Sokoni umetua katika Bonde la Ufa ambapo kampuni ya mawasiliano ya Safaricom ikishirikiana na Royal Media Services imeendelea na kampeni za MPESA mashinani. Watangazaji wa Radio Citizen na Chamgei FM waliwasilisha ujumbe wa shamrashamra za kusherehekea miaka 18 ya huduma za MPESA.