Mgonjwa mwingine amefariki ndani ya wodi KNH - Citizen TV Kenya
Mgonjwa mwingine alipatikana ameuawa ndani ya wodi 7B katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta. Ripoti za awali zinaashiria kuwa mgonjwa huyo wa umri wa miaka 54 aliuawa akiwa kitandani alikokuwa amelazwa. Maafisa wa DCI wanaendelea na uchunguzi baada ya mshukiwa mmoja ambaye ni mgonjwa katika hospitali hiyo kukamatwa na kuzuiliwa kwa kisa cha jana