Mchuano wa voliboli ya walemavu wang'oa nanga ugani Kasarani, Nairobi

5 hours ago 1


Mchuano wa Afrika kwa voliboli ya walemavu umeanza rasmi katika uwanja wa Kasarani hapa Nairobi. Kwa sasa timu ya taifa ya Kenya kwa wanawake inachuana na Rwanda ambazo ndio timu pekee upande wa wanwake. Hii ikimaanisha timu zote mbili zimetinga kwa mchuano wa dunia utakaoandaliwa nchini Marekani. Kwenye mechi ya awali Misri iliinyeshea Afrika Kusini seti tatu kwa bila huku ile ya Kenya ikitarajiwa kupambana na Algeria baadae usiku wa leo. Jumla ya mataifa nane yanashiriki mchuano huu.
Open Full Post