Mashahidi 6 wametoa ushahidi kwenye kesi ya sakata ya masomo nchini Finland

18 hours ago 2


Mashahidi sita wamekuwa wa punde zaidi kueleza masaibu yao kwenye kesi ya ulaghai wa ufadhili wa masomo nchini Finland. Kesi hii ya sakata ya shilingi bilioni moja inamuhusisha Seneta wa Uasin Gishu, Jackson Mandago, na washukiwa wenzake wawili Meshack Rono na Joshua Lelei. Shahidi wa 100 katika kesi hiyo ambaye alikuwa Mkuu wa Wafanyakazi wa Kaunti ya Baringo Edward Kiptek, alimweleza hakimu mkuu Peter Ndege jinsi alivyolipa shilingi milioni 2.5 kufanikisha masomo ya wanawe wawili. Yeye na mashahidi wengine watano waliieleza mahakama jinsi walivyolipa karo ili watoto wao waende kusoma ughaibuni kupitia mpango huo, lakini hakuna hata mmoja aliyesafiri hadi sasa. Kiptek alibanwa kueleza ni kwa nini aliwalipia wanawe wawili ilhali masharti ya mpango huo yalielekeza kila familia iruhusiwe mwanafunzi mmoja pekee.
Open Full Post