Maaskofu wa kanisa la Kianglikana nchini wanashinikiza kusitishwa kwa maandamano
Maaskofu wa kanisa la Kianglikana nchini wanashinikiza kusitishwa kwa maandamano wakisema kuwa yanatumiwa na wahuni kuzua vurugu. Maaskofu hao wanasema kuwa japo ni haki ya wakenya kuandamana, maafa mengi yametokana na maandamano. Kwenye taarifa, maaskofu hao pia wametaka mikutano ya kisiasa inayoendelezwa na viongozi wa serikali na wa upinzani nchini kusitishwa wakisema yanachochea uhasama badala ya kuhamasisha umma.