Kwale: Raymond Omollo asaidia ukuaji wa vipaji - Citizen TV Kenya
Vijana kaunti ya Kwale wametoa wito kwa viongozi na washikadau wa michezo kuwasiadia kukuza vipaji vyao kwa kuwapa vifaa vinavyofaa pamoja na ukarabati wa viwanja. Wakizungumza katika uwanja wa maonyesho wa Ukunda baada ya kupokea vifaa kutoka kwa katibu wa usalama Raymond Omolo, wachezaji wa timu za Amsterdam na kombani wamewataka viongozi wao kuiga mfano wa katibu huyo ili pia kupiga vita uhalifu miongoni mwa vijana na utumizi wa mihadarati. Wakfu huo unaendeleza zoezi la kugawanya sare za mpira kwa kaunti zote 47 ili pia kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao.