Harambee Stars yawasilisha Arusha kwa mchuano wa mataifa manne - Citizen TV Kenya

1 day ago 110


Timu ya taifa soka Harambee Stars imefika jiji Arusha Tanzania tayari kwa mchuano wa mataifa manne kujiandaa kwa dimba la CHAN. Stars iliondoka nchini asubuhi ya leo kwa ndege ya kibinafsi baada ya kuwa kambini kwa siku kumi. Mshambulizi wa Bandari Beja Nyamawi ameachwa nje ya msafara huo kutokana na jeraha huku Masud Juma akiitwa mahali pake. Kenya itaanza mchuano huo dhidi ya Uganda siku ya Jumatatu na kisha Tanzania na Senegal mtawalia.
Open Full Post