Gavana wa Kajiadi Ole Lenku akemea wahuni waliovamia hospitali
Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku amejitokeza na kushutumu vikali uvamizi wa hospitali ya Kitengela Level 4 wakati wa maandamano ya siku ya saba saba, ambapo uharibifu mkubwa ulishuhudiwa. Akizungumza baada ya kukagua uharibifu huo Lenku anasema waliotekeleza uhalifu huo hawakuwa waandamanaji ila wahuni ambao wanapaswa kukabiliwa kisheria