Fisi amuua kijana Njoro, wakazi walia kuhusu Mashambulizi - Citizen TV Kenya
Huzuni na simanzi imetanda katika Kijiji cha Sinendet, eneo la Njoro, Kaunti ya Nakuru, baada ya mvulana wa miaka 14 kuuawa na fisi. Kijana huyu alitoweka kabla ya mabaki ya mwili aftermath kupatikana. Wakaazi wa eneo hili wakilalamikia kuongezeka kwa visa vya uvamizi wa fisi.