DCIO wa Nairobi Central awasilisha ushahidi wa mauaji wa Rex Masai - Citizen TV Kenya
Afisa wa upelelezi wa jinai wa Nairobi Central, Tiberius Ekisa, amekana kumfahamu Isiah Murangiri, afisa wa polisi ambaye ni mshukiwa mkuu w amauaji ya Rex Masai aliyefariki kwenye maandamano ya kupinga mswada wa fedha mwaka jana jijini Nairobi. Ekisa ameieleza mahakama kuwa Isiah Murangiri, hakuwa chini ya amri yake tarehe 20 mwezi Juni mwaka jana wakati ambapo Rex aliuwawa