Albert Ojwang azikwa nyumbani kwao Homa Bay

1 day ago 4


Viongozi kutoka Nyanza wamekemea wahuni ambao wamehusika katika kuvuruga maandamano ya amani ya kizazi cha Gen Z hapa nchini. Wakizungumza huko Homa Bay wakati wa mazishi ya mwalimu na Mwanablogu Albert Ojwan'g, viongozi hao wamewataka Gen Z kutokubali ajenda yao kuingiliwa na wahuni wanaovuruga amani na kuharibu mali. Wakati huo huo familia ya Albert Ojwan'g imewataka wakenya wasiache kupigania haki ya Ojwan'g kwa wahusika wa mauaji yake.
Open Full Post